Kikosi chaTwiga Stars leo kinashuka dimbani kusaka tiketi ya kufuzu mashindano ya Olimpiki
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime, amesema wanahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujihakikishia nafasi
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa hatua ya pili dhidi ya Botswana kuwania kufuzu Olimpiki mwakani nchini Ufaransa, mchezo utakaochezwa kuanzia saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Azam Complex
Shime amesema amekaa na wachezaji wake kuwaandaa kimbinu na kisaikolojia ili kuweza kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani