Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 30 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 30 2023

Roma wanafikiria kumkabidhi mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 26, kwa klabu yake zamani ya Chelsea katika mkataba wa kubadilishana mshambuliaji wa The Blues na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Italia. (Mirror)

Real Madrid inapanga kuwasajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, kutoka Paris St-Germain na mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 23. Klabu hiyo ya Uhispania inanuia kumsaini mchezaji huyo wakati kandarasi yake itakapokamilika msimu ujao. (El Chiringuito, via 90 min)

Arsenal, Manchester United na Manchester City zote zina nia ya kumsajili beki wa Crystal Palace na Uingereza Marc Guehi, 23. (Goal)

Chelsea itamsaka beki na mshambuliaji katika dirisha la usajili la Januari. (Fabrizio Romano)

Arsenal wako tayari kumuuza kipa wa England Aaron Ramsdale msimu ujao baada ya kubadili nia yao kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Fluminense Mbrazil Andre Trindade, 22, anasema alikataa kuhama msimu wa joto, huku Liverpool na Arsenal zikiwa na nia ya kusaidia timu yake kushinda Copa Libertadores. (90 min)

Liverpool wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Bayern Munich Mjerumani Jamal Musiala, 20, ambaye hajaridhishwa na muda anaopewa kucheza na anachukuliaLigi ya Premia kama mahali pa kuvutia. (Mirror)

Aston Villa wanajiandaa kuanza mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa Brazil Douglas Luiz, 25, ambaye Arsenal wanamhusudu. (Football Insider)

Manchester United wanavutiwa na mchezaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 na beki wa Nice Jean-Clair Todibo. (Fabrizio Romano)

Arsenal na Tottenham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 27, lakini hawako tayari kulipa dau la pauni milioni 61. (Fichajes - kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Uingereza Jesse Lingard anatafuta klabu mpya kwa sababu Al-Ettifaq hawana nafasi katika kikosi chao. (Star)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
21h ago
READ MORE β†’