Azam Fc imemuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Yahya Zaid
Zaid ni mmoja wa wachezaji waandamizi wa kikosi cha Azam Fc ambapo kwa nyakati tofauti alikwenda kucheza soka la kulipwa nchini Misri kisha kurejea tena Azam Fc
"Tumeingia mkataba mpya wa miaka miwili na kiungo wetu mshambuliaji, Yahya Zaid, utakaomfanya kuendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026," ilibainisha taarifa fupi ya Azam Fc
Zaid amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Azam Fc msimu huu