Messi aweka rekodi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 31st October 2023


Messi aweka rekodi

Usiku wa kuamkia leo, mchezaji Lionel Messi alishinda kwa mara ya nane tuzo ya mwaka huu ya mchezaji bora wa soka duniani "Ballon d'Or"

Sherehe za kutangazwa kwake zilifanyika jana usiku mjini Paris Ufaransa

Messi mwenye umri wa miaka 36 na ambaye alishinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya kwanza mwaka 2009, amewapiku Erling Haaland aliyechukua nafasi ya pili, Kylian Mbappe nafasi ya tatu. Mchezaji raia wa Ubelgiji Kevin de Bruyne akishika nafasi ya nne

Mafanikio ya Messi ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Inter Miami baada ya msimu mbaya katika timu ya Paris Saint Germain, yametokana hasa na kuiwezesha timu yake ya taifa ya Argetina kutwaa Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana, baada ya kuishinda Ufaransa kwa mikwaju ya penati


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.