Baada ya kupoteza mechi mbili zilizopita, Azam Fc imezindukia mkoani Kigoma wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ihefu Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika
Mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Kipre Junior, Gibril Sillah na Lasane Diarra yalitosha kuihakikishia Azam Fc ushindi muhimu uliowarejesha katika nafasi ya tatu baada ya kufikisha alama 16
Kiungo fundi wa Azam Fc Feisal Salum 'Fei Toto' leo alikuwa na mchango mkubwa katika ushindi huo akitoa pasi za mabao mawili
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Mashujaa kupoteza katika uwanja wao wa nyumbani
Timu hiyo ilianza vyema nyumbani msimu huu ikishinda mechi mbili na kutoka sare mchezo mmoja
Mashujaa ilipoteza mechi mbili ilizocheza ugenini kabla ya kumenyana na Azam Fc leo
Katika mchezo mwingine uliopigwa mapema, Singida BS ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ihefu Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa LITI