Simba - Yanga - Azam - Taifa Stars - Tanzania - Local

Ligi ya Muungano kurejeshwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Nov 2023
Ligi ya Muungano kurejeshwa

Serikali iko mbioni kurudisha Ligi ya Muungano lakini imetoa sababu ya kukosa ufadhili kwamba limekuwa ni tatizo

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Alhamisi Novemba 2, 2023 na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma wakati ajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Magomeni (CCM) Mwanakhamisi Kassim Said.

"Serikali ipo kwenye mchakato wa kurudisha Ligi ya Muungano na mapema tutairudisha, tatizo litakuwa kwenye udhamini kwani ndiyo kitu tunachokitafuta kwa sasa,” amesema Mwinjuma.

Aidha Mh Mwinjuma amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imekuwa ikishirikiana na ZFF katika mipango mbalimbali kwa lengo la kuendeleza Soka la Tanzania.

Naibu Waziri amesema kwa sasa Bodi ya Ligi ipo katika mchakato wa kuandaa mafunzo ya uendeshaji wa Bodi ya Ligi ya Zanzibar ambayo kimsingi yatalenga namna ya uendeshaji wa Bodi ya Ligi katika masuala ya Menejimenti, Ligi na masuala ya uwekezaji, udhamini na masoko.

Naibu Waziri amesema kwa upande wa kuibua vipaji, TFF imekuwa ikishirikiana na ZFF katika uteuzi wa wachezaji katika timu za Taifa za vijana, ambapo vijana kutoka Zanzibar wamekuwa wakiitwa katika vikosi vya timu ya Taifa ya vijana na hatimae kucheza katika timu ya Taifa ya wakubwa Taifa Stars.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’