Yanga - Simba - Singida - Azam - Local

Mudathir, Feisal wanusurika kifungo kutoka TPLB

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Nov 2023
Mudathir, Feisal wanusurika kifungo kutoka TPLB

Wachezaji Mudathir Yahya wa Yanga na Feisal Salum (Fei Toto) wa Azam wametozwa faini ya Sh2 milioni kila mmoja kwa kosa la kukataa kupeana mikono na waamuzi na wachezahu kabla ya mechi ya Yanga vs Azam kuanza Oktoba 22 Uwanja wa Mkapa

Katika taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza wachezaji hao walisimama katika mstari wa kuingia kiwanjani muda wa kupeana mikono kisha kuingia baada ya zoezi hilo kukamilika

Katika mechi hiyo mwamuzi namba moja, Janeth Balama wa Iringa amesimamishwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu

Aidha, mshambuliaji wa Singida Big Stars, Habib Kyombo ametozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina katika mechi dhidi ya Namungo

Bodi ya Ligi pia imeelezwa kusikitishwa na kitendo cha ukatili na vurugu kilichofanywa na mashabiki waliokuwa wamevaa jezi ya Simba na bluu kumshambukia shabiki wa Yanga katika mechi ya Simba vs Ihefu Uwanja wa Mkapa

Bodi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama inakamilisha mchakato wa kuwatambua mashabiki wote waliohusika na tukio hilo kabla ya kuwachukulia hatua kali

Katika ligi ya Championship, Mchezaji Gilbert Boniface wa Cosmopolitan inayoshiriki Ligi ya Championship nchini Tanzania amefungiwa mechi 10 na faini Sh500,000 kwa kosa la kumshika mwamuzi sehemu za siri kwenye mechi dhidi ya Ken Gold wakati akipinga maamuzi ya mwamuzi huyo

"Baada ya tukio hilo mwamuzi alimuonyesha kadi nyekundu mchezaji huyo, ambaye alimfata na kumpiga teke kabla ya kutoka nje," imeeleza taarifa ya Bodi ya Ligi

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
39m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
51m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’