Yanga - Local

Gamondi aipania Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Nov 2023
Gamondi aipania Simba

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ana matumaini makubwa kikosi chake kitafanya vizuri kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumapili kaatika uwanja wa Benjamin Mkapa

Gamondi amesema amekuwa na wiki nzuri ya maandalizi, wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo

"Ninafurahi kuwa sehemu ya mchezo huu, tumejiandaa vizuri na tumekuwa na wiki nzima ya maandalizi. Nina imani na wachezaji wangu, kesho tutakuwa na mchezo mzuri, kila mshabiki wa soka atafurahia mchezo"

"Ni wazi mchezo wa kesho utakuwa tofauti na mchezo wa kwanza tuliocheza kwenye Ngao ya Jamii. Tunacheza katika uwanja mzuri na kila timu iko katika kiwango bora baada ya kucheza mechi kadhaa za ligi"

"Tunahitaji kushinda mchezo huu kwa sababu alama tatu zitatuhakikishia kuwa juu ya msimamo wa ligi. Najua ni derby lakini kwangu ni alama tatu muhimu," alisema Gamondi

Gamondi amesisitiza kikosi chake kina wachezaji bora na wenye uzoefu na ana matumaini makubwa watashinda mchezo huo

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinzi wa kati Dickson Job amesema wamejiandaa vyema kuwania alama tatu katika mchezo huo

"Kwa upande wetu wachezaji tuko tayari kwa asilimia 100, walimu kwa upande wao wamemaliza kile walipanga kutuelekeza, imebaki kwetu wachezaji kutekeleza uwanjani," alisema Job

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’