Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Novemba 6 2023

Joel JJ By Joel JJ
6 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Novemba 6 2023

Arsenal wako tayari kumpa mlinzi wa Uingereza Ben White nyongeza kubwa ya mshahara huku wakitarajia kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 chini ya mkataba mpya na ulioboreshwa katika klabu hiyo (Football Insider)

Liverpool na West Ham zote zinatazamia kumnunua kiungo wa kati wa Napoli raia wa Poland Piotr Zielinski, 29, ambaye mkataba wake unaisha msimu huu wa joto (Teamtalk kupitia Corriere dello Sport)

Luton bado wana matumaini ya kumnunua kiungo wa kati wa Ecuador mwenye umri wa miaka 19 Oscar Zambrano, ingawa mchezaji huyo wa LDU Quito anaweza kusalimisha sehemu yake ya ada ya uhamisho. (Sun)

Mabeki wa Uhispania Marcos Alonso, 32, na Sergi Roberto, 31, hawatapewa kandarasi mpya na Barcelona . (Sport - kwa Kihispania)

Real Madrid hawatafanya usajili mpya katika dirisha la usajili la Januari. (Fichajes - kwa Kihispania)

Meneja wa Al-Ettifaq Steven Gerrard amedokeza kuwa timu yake itavamia vilabu vya Ulaya kwa mara nyingine tena mwezi Januari kutafuta wachezaji wapya (Goal)

Barcelona wanaaminika kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya mlinzi wa Ufaransa aliye kwa mkopo Clement Lenglet katika Aston Villa , huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa bado hajacheza Ligi ya Premia. (Sport - kwa Kihispania)

Real Madrid wanatumai urafiki ambao fowadi wa Brazil Vinicius Junior, 23, anao na nyota wenzake unaweza kuwa ufunguo wa kupata usjili wa baadaye wa wachezaji kama beki wa Canada wa Bayern Munich Alphonso Davies, 23, na mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, 24. ( AS - kwa Kihispania)

Nyota wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri amemshauri Mbappe abaki Ufaransa badala ya kuelekea Madrid msimu ujao wa joto. (Le10Sport - kwa Kifaransa)

Kocha mkuu wa Atletico Madrid Muargentina Diego Simeone anakaribia kuongezewa mkataba na klabu hiyo ya La Liga hadi angalau 2027. (Marca).

BBC

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
54m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
57m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →