Yanga - Local

Gamondi azitaka alama tatu dhidi ya Coastal Union

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Nov 2023
Gamondi azitaka alama tatu dhidi ya Coastal Union

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Mkwakwani

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mkoani Tanga leo, Gamondi alisema licha ya ugumu wa ratiba, wamejipanga kushinda mchezo huo

Gamondi amesema kikosi chake kilipata muda mchache wa kufanya mazoezi ya kurejesha utimamu wa mwili baada ya mchezo dhidi ya Simba na baadae kusafiri kuelekea Tanga

Leo watafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkwakwani tayari kwa mchezo huo ambao wanafahamu umuhimu wake

"Sina mengi ya kuzungumza kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Coastal Union kwasababu ya muda, jana tumetumia siku yetu kwa ajili ya kurudisha miili sawa na kusafiri kuja Tanga. Na leo tutakuwa na mazoezi kidogo jioni hayo ndio ninayoweza kusema kwa sasa"

"Michezo inayokuwa kwenye siku za karibu kwenye ligi ina changamoto hasa unapotoka kwenye mechi ngumu na kusafiri lakini Wachezaji wetu wako tayari na wote tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho," alisema Gamondi

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’