Simba - Namungo - Local

Simba yapania kumaliza hasira kwa Namungo Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Nov 2023
Simba yapania kumaliza hasira kwa Namungo Fc

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Daniel Cadena amesema wachezaji wana ari na morali kubwa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Uhuru

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Cadena alisema amezungumza na wachezaji wote, amewataka wasahau matokeo yaliyopita sasa ni wakati wa kuanza upya na kuwa bora zaidi

"Kabla sijaanza majukumu yangu, nilizungumza na wachezaji na kuwauliza kama wanataka niwe kocha wao au la? Kwa pamoja walisema wananihitaji kuwa kocha wao"

"Nikawaambia sasa tunapaswa kufanya kazi, tusahau matokeo ya mchezo uliopita, tuanze upya kwa kuboresha zaidi"

"Nafurahi kuona baada mazungumzo yetu kila mchezaji alikuwa tayari, wamefanya mazoezi kwa ari kubwa na wameonyesha wako tayari kwa mchezo dhidi ya Namungo ambao malengo yetu ni kupata ushindi," alisema Cadena

Akizungumza hali ya kiungo mshambuliaji Kibu Denis, Cadena amesema Kibu alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Yanga lakini jana alianza mazoezi mepesi ya Gym

"Kibu ni mchezaji muhimu katika kikosi chetu, alipata majeraha kwenye mchezo uliopita, nimetaarifiwa na daktari wa timu kuwa anaendelea vizuri na jana alianza mazoezi ya Gym"

"Tutamuangalia baada ya mazoezi ya mwisho leo kuona yuko tayari au la. Lakini Simba ina wachezaji wengi ambao wote wana umuhimu. Hatutaangalia majina ya wachezaji, atakayepata nafasi ni yule ambaye anatuonyesha katika kiwanja cha mazoezi kuwa yuko tayari," alisema Cadena

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’