Local - Simba - Yanga - Azam - Singida

Timu za Bara ruksa kutumia uwanja wa Amaan Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Nov 2023
Timu za Bara ruksa kutumia uwanja wa Amaan Zanzibar

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma mwanafa amesema hakuna kikwazo kwa Timu yoyote ya Ligi Kuu kuchagua Uwanja wa Nyumbani katika mechi zake ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mhe Mwinjuma amebainisha kuwa kabla ya Ligi Kuu ya Tanzania kuanza Timu zina uhuru wa kuchagua uwanja wa nyumbani utakaotumika kwenye michezo ya timu husika ndani ya Tanzania Bara au Zanzibar bila kuathiri Kanuni na miongozo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Tanzania na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF).

Mhe. Mwinjuma amesema hayo Novemba 8, 2023 Bungeni Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati akijibu Swali la Mhe Mussa Omar Salim (Gando) aliyeuliza Je, kwa nini baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya Tanzania zisichezwe kwenye Viwanja vya Gombani na Amani vilivyopo Pemba na Unguja.

"Endapo timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu itawiwa kutumia Uwanja vya Gombani na Amani Zanzibar kama Uwanja wa nyumbani hakutakua na kikwazo chochote ikiwa timu itakidhi makubaliano na uongozi unaosimamia taratibu na matumizi ya uwanja husika bila kuathiri Kanuni na miongozo ya TFF na Bodi ya Ligi Tanzania" amesisitiza Mhe.

Mwinjuma. Ameongeza kuwa, Kanuni ya 9:7 ya Bodi ya Ligi inaruhusu timu ya Ligi Kuu kuteuwa viwanja vingine miongoni mwa Viwanja visivyotumika katika mchezo wa Ligi Kuu kwa michezo yake miwili tu ya Nyumbani na kuwasilisha uteuzi wake siku ishirini na moja kabla ya mchezo husika unaokusudiwa kuchezwa kwenye Uwanja ulioteuliwa.

Akijibu Swali la Nyongeza la Mhe. Festo Sanga kuhusu kurejesha Ligi ya Muungano, Naibu Waziri Mhe. Mwinjuma amesema tayari Wizara zinazosimamia michezo zimeshaanza utaratibu kupitia TFF na ZFF wa kurejesha ligi hiyo ambayo ni Ligi inayounganisha Watanzania na kudumisha Muungano bila kuathiri ratiba ya Ligi Kuu.

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
1h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
5h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
6h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
8h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
8h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’