Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema mchakato wa kutafuta mrithi wa Kocha Robertinho Oliveira umeanza mara moja na utakamilishwa mapema
Ahmed amesema mkakati wa Simba ni kuhakikisha kocha anajiunga na timu haraka kabla ya mechi za hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi unatarajiwa kupigwa Novemba 25, ambapo Simba itaumana na ASEC Mimosas katika uwanja wa Benjamin Mkapa
"Tuna takribani wiki mbili kabla ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya ASEC Mimosas, uzuri baada ya mchezo wetu dhidi ya Namungo Fc ligi itasimama kupisha mechi za Kimataifa zilizo kwenye kalenda ya FIFA"
"Mkakati wetu ni kumpata kocha mapema ili atumie kipindi cha mapumziko ya FIFA kuiandaa timu kwa ajili mechi za hatua ya makundi ligi ya mabingwa"
"Hivyo niwahakikishie tu, mchakato uko mbioni kukamilika na kila kitu kikiwa sawa tutamtangaza kocha wetu mpya ambaye atakuja kuendeleza alipoishia Robertinho," alisema Ahmed