Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi hana muda wa kupoteza kwani kikosi chake kimeanza maandalizi ya mchezo wa ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya CR Belouzdad
Yanga iko kundi D sambamba na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, CR Belouzdad ya Algeria na Medeama ya Ghana
Gamondi amepania kuipa Yanga mafanikio makubwa katika michuano hiyo akiamini timu yake ina wachezaji bora wanaoweza kushindana na timu yoyote barani Afrika
Kocha huyo raia wa Argentina amebainiha kuwa ubora wa kikosi chake unatokana na mambo mengi huku akitaja kuwajibika kwa kila mmoja kuwa ndio silaha yao kubwa
"Yanga kuanzia benchi la ufundi, wachezaji na viongozi tumekuwa wamoja hii ni njia bora na ya kujenga pamoja ili kuweza kufikia mafanikio jambo ambalo hadi tulipofikia sasa tunaona mwanga"
"Akili yote sasa imehamia kimataifa tunataka kuweka rekodi nyingine baada ya kutinga hatua ya makundi baada ya miaka 25 malengo sasa ni kusonga mbele zaidi kwa kucheza robo fainali," alisema Gamondi