Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Novemba 11 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Novemba 11 2023

Real Madrid wanaweza kujaribu kumnunua mshambuliaji wa Manchester City na Norway, Erling Haaland, 23. Dau la kumnunua Haaland linatazamiwa kufikia Euro milioni 200 (£174m) kufikia mwishoni mwa msimu huu.

Pindi tu uchukuaji wake wa asilimia 25 wa Manchester United utakapokamilika, Sir Jim Ratcliffe atataka kumuuza mshambuliaji Mfaransa Anthony Martial, 27, winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, na winga wa Brazil Antony, 23. (Mirror).

United wanaweza kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, huku mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 24 wa Paris St-Germain ukikamilika mwaka ujao. (Football Insider)

Real Madrid inasalia kuwa kimbilio la Mbappe endapo ataondoka PSG, lakini timu hiyo ya Uhispania itakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu kadhaa vya Premier League vikiwemo Manchester City, Newcastle United, Chelsea na Liverpool. (TeamTalk)

Ratcliffe anataka kujua jinsi Manchester United imetumia £1.4bn kwenye uhamisho katika muongo mmoja uliopita - lakini anaamini kuwa meneja Erik ten Hag bado ana mkopo benki huku msimu huu ukiwa na mwanzo mbaya. (Sun)

Manchester City wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa West Ham wa Brazil Lucas Paqueta, 26, ambaye meneja Pep Guardiola anamwona kama mrithi anayetarajiwa wa mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 32. (UOL, via MEN)

Kipa wa kimataifa wa Uhispania na mlinda mlango wa zamani wa Manchester United David de Gea, 33, yuko tayari kujiunga na klabu ya La Liga Real Betis kwa mkataba wa muda mfupi. (El Desmarque - in Spanish)

Barcelona wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Corinthians, Gabriel Moscardo, 18, mbele ya Chelsea, ambaye hamu yake ya kumsajili Mbrazil huyo msimu uliopita iliambulia patupu, na Arsenal. (90min)

Liverpool wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Leeds United na Uingereza Archie Gray, 17, ambaye anaweza kugharimu zaidi ya £40m. (Mail)

Licha ya kupunguzwa kwa chaguo lao la beki wa kati, Tottenham Hotspur haiwezi kumrejesha mlinzi wa Wales Joe Rodon, 26, kutoka katika kipindi chake cha mkopo cha msimu mzima akiwa Leeds United. (The Athletic)

Mshambulizi wa Brazil Neymar huenda akafutiwa usajili na klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kutolewa nje msimu huu kutokana na jeraha. (Arriyadiyah, via Goal)

Bayern Munich wanatazamiwa kushinda katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Australia Nestory Irankunda, 17 kutoka Adelaide United ya A-League. (ESPN)

West Ham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen wa Nigeria Victor Boniface, 22, huku The Hammers pia wakifikiria nafasi ya meneja David Moyes. (TeamTalk)

Newcastle United inamfuatilia beki wa kati wa Lille Mreno Tiago Djalo mwenye umri wa miaka 23 - lakini anaweza kukabiliwa na ushindani kutoka vilabu kadhaa vya Uropa vikiwemo Inter Milan, Juventus na Barcelona. (90min)

Vinginevyo, Moyes anatarajiwa kuendelea na mkataba wake West Ham - ambao utaendelea hadi msimu ujao - licha ya matokeo ya hivi karibuni, labda klabu hiyo ipate mgombea anayefaa zaidi. (90min)

Fulham iko tayari kumsaidia kwa kiasi kikubwa meneja Marco Silva katika dirisha la uhamisho la Januari baada ya kocha huyo Mreno kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo. (Football Insider)

Chelsea ilimsajili mshambuliaji wa Uingereza Cole Palmer, 21, kutoka Manchester City msimu huu baada ya kumkosa winga wa Ubelgiji Jeremy Doku, 21, aliyejiunga na City, na winga wa Crystal Palace Mfaransa Michael Olise. (Evening Standard)

Meneja wa Blues Mauricio Pochettino hatakuwa na ushawishi katika shughuli ya uhamisho wa Chelsea mwezi Januari. (Sun)

Meneja wa zamani wa Chelsea na Everton Frank Lampard ameibuka kuwa mgombea anayeongoza kuchukua mikoba ya klabu ya League One ya Oxford United. (Portsmouth news)

Watunga sheria za kandanda wameanza mazungumzo juu ya mabadiliko makubwa ya jinsi waamuzi wasaidizi wa video wanavyofanya kazi - na uangaliaji wa mchezaji kama ameotea kupitia machine na binadamu unaweza kuanzishwa katika Ligi ya Premier msimu ujao. (Telegraph)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’