Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Ndege maalum kwa ajili ya kukisafirisha kikosi cha timu ya Taifa ya Taifa Tanzania kwenda nchini Morocco kucheza dhidi ya Timu ya Taifa ya Niger
Rais Samia ametoa usafiri huo kwa ajili ya mchezo huo wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Kombe la Dunia
"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais, sasa timu itasafiri kwa muda mfupi kwenda Marrakesh tarehe 16 Novemba, 2023 na itarejea haraka tarehe 19 Novemba, 2023 baada ya mchezo wake wa tarehe 18 Novemba, 2023 dhidi ya Niger"
"Kisha tarehe 21 Novemba itakuwa na kibarua kingine cha kucheza na Timu ya Taifa ya Morocco katika mbio hizo hizo za kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia lijalo litakaloandaliwa na Marekani, Canada na Mexico “ ilisema taarifa iliyotolewa na Katibu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
Stars iko kambini ikiendelea na maandalizi ya mechi hizo