Klabu ya Yanga inatajwa kumuwania kiungo mkabaji tegemeo wa Racing Club ya Ivory Coast na timu ya taifa ya Ivory Coast ya vijana (U-20), Djire Abdoulaye
Djire mwenye umri wa miaka (18) amekuwa mchezaji tegemeo wa Racing Club licha ya umri wake kuwa mdogo
Kinda huyo pia anahusishwa na klabu za ASEC Mimosas na TP Mazembe
Yanga inasaka kiungo mkabaji ambaye atakuwa mbadala wa muda mrefu wa Khalid Aucho ambaye pamoja na ubora alionao, umri unamtupa mkono
Djire ni moja kati ya wachezaji waliounda Kikosi bora cha msimu cha ligi kuu ya Ivory Coast 21/22



