Simba - Local

Simba yazindua chaneli ya WhatsApp

Joel JJ By Joel JJ
14 Nov 2023
Simba yazindua chaneli ya WhatsApp

Klabu ya Simba leo imetangaza kuzindua rasmi chaneli ya whatsApp ikiwa klabu ya kwanza kufikia hatua hiyo

Akizungumza katika mkutano na Wanahabari mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula alisema Simba ikiwa klabu yenye wafuasi zaidi kwenye mitandao kijamii kuliko klabu yoyote Tanzania, kupia WhatsApp Wanasimba watakuwa karibu zaidi ya timu yao kwa kupata taarifa muhimu kwa haraka

"Instagram tuna watu zaidi ya 5.5 milioni, Facebook zaidi ya 1.9 milioni, Twitter zaidi ya 1.5 milioni, YouTube tukiwa na zaidi ya 438k, kwenye app imepakuliwa zaidi ya laki saba na hivi karibuni tumeshinda tuzo ya mashabiki bora."

"Leo tunazindua Simba Sports Club WhatsApp channel. WhatsApp imepakuliwa na watu Bilioni 2.2 duniani ndio mtandao umepakuliwa zaidi duniani. WhatsApp wenyewe walitufata kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na chaneli hii."

"Ni timu chache kama Kaizer Chiefs, Al Ahly, Barcelona, Real Madrid na Simba tumejiunga. Katika kuijaribu kabla ya kuzindua ndani ya wiki tumepata wafuasi laki moja. Faida kubwa ni mashabiki kupata taarifa na wadhamini wetu kuonyesha bidhaa zao."

"Hili ni lingine la kwanza kwa Simba kuwa karibu kwa Wenye Nchi. Simba inataka kuja kuwa timu namba moja Afrika na katika hili moja ya sehemu ya kuboresha ni namna ya kutoa habari."

"Tunapokuwa na chaneli kama hivi ni sehemu ya Wanasimba na watu wengine kupata taarifa sahihi za klabu. Hii ndio klabu ambayo inafanya vitu vyenye faida na tofauti."

"Ujio wa Simba WhatsApp Channel unakuja na ajira kwa mtu maalumu kuwa na kazi ya kutoa habari," alisema Kajula

Kajula pia aligusia mchakato wa kupatikana kocha mpya ambapo amesema mchakato huo uko kwenye hatua za mwisho

"Kuhusu kocha tupo kwenye mchakato wa mwisho"

SIMBA WHATSAPP CHANEL

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
52m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
55m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →