Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi, Novemba 16 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi, Novemba 16 2023

Newcastle United wanamtaka mshambuliaji wa Uhispania Ferran Torres, ambaye Barcelona wanajiandaa kumuuza baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City, 23, kushindwa kufikia matarajio ya klabu hiyo ya La Liga. (Fichajes - Kwa Kihispania)

Chelsea, Liverpool na Manchester City wanamuwania beki wa Bayern Munich Alphonso Davies,23, lakini wanaamini mchezaji huyo anatamani sana kujunga Real Madrid. (90min)

Newcastle wanatafakari uwezekano wa kumnunua mlinzi wa Ujerumani na Bayer Leverkusen ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni Jonathan Tah, 27, Januari mwakani. (Sun)

Manchester United inakataa kumruhusu Jadon Sancho, 23, kuondoka kwa bei nafuu katika dirisha la uhamisho la Januari - licha ya meneja Erik ten Hag kutaka kumuondoa winga huyo wa Uingereza. (Mirror)

Chelsea wako tayari kushindana na Arsenal na Liverpool kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Corinthians mwenye umri wa miaka 18 kutoka Amerika Kusini Gabriel Moscardo, ambaye anaweza £26m. (Standard)

Chelsea wako tayari kumenyana na Arsenal na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa Corinthians mwenye umri wa miaka 18 kutoka Amerika Kusini Gabriel Moscardo, ambaye anaweza kugharimu takriban £26m. (Standard)

Mshambulizi wa Newcastle na England Callum Wilson, 31, atakuwa nje kwa karibu wiki sita kutokana na jeraha la misuli ya paja, huku mchezaji mwenzake wa Magpies, mlinzi wa Uholanzi Sven Botman, 23, akitarajiwa kuwa nje kwa muda mrefu zaidi kwa sababu ya tatizo la goti. (Telegraph - usajili unahitajika)

Manchester United wanaendelea kumfuatilia mshambuliaji wa Brighton Evan Ferguson, 19, licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland hivi karibuni kusaini mkataba mpya na Seagulls. (Football Insider)

Mkurugenzi wa RB Leipzig Rouven Schroder amefungua mlango kwa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Timo Werner mwenye umri wa miaka 27 kuondoka katika klabu hiyo, huku Mjerumani huyo akiwa ameanza mechi mbili pekee msimu huu. (Standard)

Kuna mashaka kuhusu mustakabali wa mkurugenzi wa kandanda wa Manchester United John Murtough na mkurugenzi wa uendeshaji wa soka David Harrison kufuatia tangazo kwamba mtendaji mkuu Richard Arnold ataondoka katika klabu hiyo. (Mirror)

BBC

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’