Barcelona - International

Alaves matatani Hispania

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Nov 2023
Alaves matatani Hispania

Beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves atatinga mahakamani Hispania kujibu mashtaka ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa mwanamke mmoja katika klabu iliyopo Barcelona Disemba mwaka jana

Alves mwenye umri wa 40 alikamatwa Januari 20 na kusota jela iliyopo nje ya Barcelona. Iwapo atapatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka minne hadi 15 jela

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Brazil, ambaye pia aliwahi kuzichezea Sevilla, Juventus na PSG, amekana kufanya makosa hayo

Katika hati iliyosainiwa na majaji watatu, mahakama ya upelelezi namba 15 huko Barcelona, ilisema kuna sababu za kutosha kwa Alves kujibu mashtaka, kufuatia maombi ya mwendesha mashtaka wa umma na mwanamke huyo

Chini ya sheria ya ridhaa masuala ya kijinsia huko Hispania iliyopitishwa mwaka jana unyanyasaji wa kijinsia unachukua nafasi kubwa kwani ni uhalifu ambao haukubaliki kwenye jamii

Alves alisema hapo awali baada ya kukamatawa: "Itathibitishwa kuwa sina hatia na yalikuwa mahusiano ya makubaliano. Haiingii akilini eti nimelazimisha tendo la ndoa"

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’