Nyota kutoka Azam Fc Academy Cyprian Kachwele amesajiliwa na klabu ya White Caps Fc ya Canada ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS)
Azam Fc imethibitisha uhamisho wa mchezaji huyo wakimtakia kila la kheri
"Tunamtakia kila la kheri mshambuliaji wetu chipukizi, Cyprian Kachwele, aliyejiunga na timu yake mpya ya Vancouver Whitecaps inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS)"
"Kachwele, amelelewa kwenye kituo chetu cha Azam FC Academy kabla ya kupandishwa timu kubwa mwishoni mwa msimu uliopita na kucheza baadhi ya mechi, akifunga mabao matatu katika mechi za mashindano"
All the best champion boy!Β
ADVERTISE HERE