Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo Jumamosi, saa 1 usiku watashuka dimbani huko Morocco kumenyana na Niger katika mchezo wa kuwania tiketi ya kombe la Dunia 2026
Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Tanzania ambayo iko kundi E sambamba na Zambia, Morocco, Niger, Congo na Eritrea iliyojiondoa katika michuano hiyo
Ukiwatoa Morocco, timu nyingine ni kama zina nafasi sawa katika kuwania kumaliza nafasi mbili za juu ili kutinga hatua ya play-off
Ushindi dhidi ya Niger ugenini yatakuwa matokeo bora kwa Stars kabla ya mchezo utakaofuata dhidi ya Morocco utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku tatu baadae
Kila la kheri Stars.....!



