Manchester United inajiandaa kuliuza kundi jingine la wachezaji 2024, huku zaidi ya wachezaji 10 wakitarajiwa kuondoka katika madirisha mawili ya uhamisho yajayo. (MEN) Kiasi cha wachezaji 15 wanaweza kuondoka United, huku winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, akitarajiwa kuwa wa kwanza kuondoka mwaka ujao. (Star)
Manchester City wanafanya kazi ya kumshawishi mshambuliaji Erling Haaland, 23, kusaini mkataba mpya, lakini makubaliano na mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway hayajakaribia. (TeamTalk)
Newcastle United wanafuatilia hali ya Dominic Calvert-Lewin huko Everton huku mshambuliaji huyo wa Uingereza, 26, akiwa kwenye orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuwindwa msimu ujao. (TeamTalk)
Fulham wamewazidi Liverpool na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Fluminense wa Brazil Andre, 22, huku mshambuliaji wa Wolfsburg Mdenmark Jonas Wind, 24, pia akiwa miongoni mwa walengwa na klabu hiyo. (Standard)
Chelsea inawafuatilia mshambuliaji wa Feyenoord na Mexico Santiago Gimenez, 22, na winga wa Real Betis kutoka Senegal Assane Diao, 18, kwa kutarajia dirisha la uhamisho la Januari. (Football Transfers)
Arsenal wameamua kusajili mshambuliaji mpya mwaka 2024 - lakini biashara hiyo inaweza kusubiri hadi dirisha refu la majira ya kiangazi. (Football Insider)
Mazungumzo ya kiungo wa kati wa Italia Jorginho ya kuongeza mkataba na Arsenal yamekwama, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (mail)
Beki wa Club America na Uruguay Sebastian Caceres, 24, ameibuka kama usajili wa kipaumbele wa Tottenham katika dirisha la uhamisho la Januari. (football.London)
AC Milan wana nia ya kutaka kumnunua kwa mkopo beki wa Chelsea Benoit Badiashile mwenye umri wa miaka 22 wa Ufaransa, huku klabu hiyo ya Italia pia itawasiliana na Arsenal kuhusu kupatikana kwa mlinzi wa Poland Jakub Kiwior, 23. (Calciomercato - in Italian).
Chelsea wako tayari kumuuza mlinzi wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24. (Football.London)
Manchester United inaweza kupigwa marufuku kutoka Uropa msimu ujao kutokana na ununuzi wa klabu hiyo na unaotarajiwa kufanywa na Sir Jim Ratcliffe, ambaye kundi lake la Ineos pia linamiliki klabu ya Nice ya Ufaransa. (Sun)
Kampuni ya uwekezaji ya Marekani ya 777 Partners inajiandaa kuingia tena kwenye mazungumzo na Everton kuhusu bei ya kuinunua baada ya klabu hiyo kupunguziwa pointi katika Ligi ya Premia. (Football Insider)
FA imethibitisha kuwa inachunguza madai ya ukiukaji mkubwa wa sheria za mawakala katika uhamisho unaohusisha Tottenham, Portsmouth na mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Jermain Defoe. (Times – Subscription Required)
BBC