Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Novemba 24 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Novemba 24 2023

Real Madrid wako tayari kutumia pesa msimu ujao baada ya kuelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 24, na mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 23. (AS - in Spanish)

Beki wa kushoto wa Chelsea Ian Maatsen, 21, yuko tayari kujiunga na Manchester City baada ya washindi hao wa mataji matatu kuhusishwa na kutaka kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi chini ya umri wa miaka 21. (Football Insider)

Arsenal itakataa mbinu yoyote ya kumnunua mlinzi wa Japan Takehiro Tomiyasu, 25, huku mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakimtaka. (Standard)

Arsenal pia wamekubali kufikia kipengele cha kumnunua mlinda mlango wa Brentford David Raya, 28, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania akitarajiwa kuwa mchezaji wa kudumu Januari kwa £27m. (Fabrizio Romano)

Manchester United, Arsenal na klabu kadhaa za Saudia vinavutiwa na winga wa Ureno Pedro Neto, 23, lakini Wolves watadai ada ya angalau £60m. (TeamTalks)

Manchester United pia wanataka kuongeza nguvu katika safu ya beki wa kati, huku mlinzi wa Nice ya Ufaransa Jean-Clair Todibo, 23, na mlinzi wa Sporting Lisbon wa Ureno Goncalo Inacio, 22, wakionekana kuwa bora kuchukua nafasi ya mchezaji wa zamani wa Ufaransa Raphael Varane, 30. (Sun).

Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 31, anaweza kuwa njiani kuondoka Manchester United mwezi Januari huku Mashetani hao Wekundu wakipania kukirekebisha kikosi chao. (TeamTalks)

Wolves pia wanakabiliwa na kibarua cha kumshikilia mlinzi mahiri Rayan Ait-Nouri baada ya Chelsea kumuongeza mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria mwenye umri wa miaka 22 kwenye orodha yao walioteuliwa. { 90min)

Chelsea wanamfuatilia winga wa Palmeiras Mbrazil Estevao Willian, 16, ambaye anasemekana kuwa na kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 52. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Winga wa Real Betis Assane Diao, 18, ameonekana kulengwa na Brentford na klabu hiyo ya Ligi ya Premia inaweza kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania chini ya umri wa miaka 21 mwezi Januari. (Sky Sports)

Newcastle na Wolves wanaweza kumgombea mlinzi wa Senegal Arouna Sangante, 21, baada ya kuvutia macho kwenye Ligue 1 akiwa na Le Havre. (Football Insider)

Wolves wamekuwa wakimsaka Mnigeria Rafiu Durosinmi, 20, lakini Eintracht Frankfurt pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Viktoria Plzen mwenye thamani ya pauni milioni 10. (Telegraph)

Barcelona wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Argentina Giovani Lo Celso, 27, huku wakitafuta hifadhi ya kiungo wa kati wa Uhispania Gavi, 19. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kocha mkuu wa Fluminense Fernando Diniz anasema kuondoka kwa kiungo wa kati wa Brazil Andre mwenye umri wa miaka 22 "kunakaribia", huku ripoti zikidai kuwa Fulham wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania saini yake. (ESPN Brazil – In Portugal)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
21h ago
READ MORE β†’