Wolverhampton Wanderers inamtaka mlinda lango wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale, 27, kwa mkopo mwezi Januari na matumaini ya kumnunua msimu wa joto (Star)
Meneja wa Nottingham Forest Steve Cooper yuko chini ya shinikizo, huku mmiliki Evangelos Marinakis akizidi kufadhaishwa na matokeo ya hivi karibuni(Mail)
Tottenham Hotspur wanavutiwa na beki wa Benfica Morato lakini klabu hiyo ya Ureno inasita kumuuza Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 22 mwezi Januari. (Record via Sport Witness)
Uwezo wa Newcastle United wa ununuzi katika dirisha la usajili la Januari utaathiriwa na iwapo mshahara wa kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali unaweza kupunguzwa huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akitumikia marufuku yake ya miezi 10 kwa kukiuka sheria za kamari. (Telegraph - usajili unahitajika)
Arsenal hawana nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Al-Hilal na Ureno, Ruben Neves, huku Mbrazil Douglas Luiz, 25, Mbrazil, akiwa mlengwa wao mkuu katika safu ya kati mnamo Januari. (Fabrizio Romano)
Tottenham wako tayari kusitisha muda wa uliosalia wa mkataba wa Hugo Lloris baada ya mlinda lango huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 36 kutofautiana na meneja Ange Postecoglou.. (Football Insider)
Real Madrid, Paris St-Germain na Manchester City wanamfuatilia mshambuliaji wa River Plate wa Argentina wa kikosi cha chini ya miaka 17 Claudio Echeverri, 17. (Sport - kwa Kihispania)
Chelsea, Liverpool na Manchester City wana nia ya kumsajili mshambuliaji chipukizi wa Italia Francesco Camarda, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza ya AC Milan Jumamosi akiwa na umri wa miaka 15. (90Min)
Fenerbahce wanavutiwa na mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 27, na watajadili mkataba na Manchester United wakati Red Devils watakaposafiri hadi Istanbul kucheza na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa. (Fotomac - kwa Kituruki)
Real Madrid wamekataa kumsajili mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi mwenye umri wa miaka 30 kutoka Galatasaray mwezi Januari. (Athletic)
Bayern Munich na Tottenham wamepunguza hamu yao ya kumnunua mlinzi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 24 Muingereza Trevoh Chalobah, ambaye yuko huru kuondoka Stamford Bridge mwezi Januari (Mirror)
Manchester United, Newcastle na Chelsea wako tayari kumnunua mshambuliaji wa Derby wa Wales, Cruz Allen, mwenye umri wa miaka 16.(Sun)
BBC