Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Novemba 27 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Novemba 27 2023

Chelsea wanatazamiwa kumfanya mshambulizi wa Napoli Victor Osimhen kuwa mlengwa wao mkuu mwezi Januari, huku mshambuliaji huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 24 akiwa tayari kuhamia Stamford Bridge.(Telegraph - usajili unahitajika)

Newcastle wanafuatilia kwa karibu ustawi wa winga wa Atletico Madrid Mbrazil Samuel Lino, 23. (Todo Fichajes - kwa Kihispania)

Juventus wana nia ya kusajili kiungo wa kati mwezi Januari na wana wachezaji watatu wa Ligi ya Premia kwenye orodha yao fupi - mchezaji wa kimataifa wa Arsenal wa Ghana Thomas Partey, 30, mchezaji wa kimataifa wa Uingereza wa Manchester City Kalvin Phillips mwenye umri wa miaka 27 na mchezaji wa kimataifa wa Denmark wa Tottenham Pierre-Emile Hojbjerg, 28. ( Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Manchester City wanataka kumsajili beki wa pembeni wa Boca Juniors Valentin Barco kabla ya kumtoa kwa mkopo kinda huyo wa kimataifa wa Argentina wa chini ya umri wa miaka 20 kwa Leicester . (Sun)

Klabu ya Saudia Al-Ettifaq inaongoza jitihada za kutaka kumsajili kipa wa Uhispania David de Gea mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ni mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita. (Sun)

West Ham wanashughulikia mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Porto wa Nigeria Zaidu Sanusi, 26, mwezi Januari. (Team Talk)

Tottenham wanafuatilia maendeleo ya mlinda lango wa Southampton wa Jamhuri ya Ireland Gavin Bazunu, 21 (Football Insider)

Liverpool wanapaswa kuilipa Benfica pauni milioni 8.5 za ziada kwa Darwin Nunez baada ya mshambuliaji huyo wa Uruguay, 24, kucheza mechi yake ya 60 katika klabu hiyo dhidi ya Manchester City Jumamosi(Mirror)

Crystal Palace na Fulham wameuliza kuhusu uwepo wa mshambuliaji wa Ajax Mwingereza Chuba Akpom mwenye umri wa miaka 28 (Team Talk) Everton wamekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Linfield wa Ireland Kaskazini, 16, Braiden Graham.. (Belfast Telegraph)

Leicester na Preston wanataka uhamisho wa mkopo wa Januari kumnunua beki wa Liverpool mwenye umri wa chini ya miaka 21, Jarell Quansah. (Alan Nixon kupitia Leicestershire Live) Winga wa West Ham wa Algeria Said Benrahma, 28, anazivutia klabu za Saudi Arabia (Sun)

Beki wa Chelsea Ian Maatsen, 21, anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa mkopo mwezi Januari ikiwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi wa chini ya miaka 21 atatia saini mkataba mpya wa muda mrefu. (Football Insider)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
56m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
4h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
19h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’