Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Disemba 04 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Dec 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Disemba 04 2023

Mshambulizi wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller, 34, amehusishwa na uhamisho wa Manchester United baada ya kutakiwa na nahodha wa zamani wa klabu hiyo ya Bavaria Lothar Matthaus kutafuta muda wa kucheza kwingineko. (The sun)

Mshambuliaji wa Juventus Matias Soule, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Frosinone, anavutiwa na Ligi ya Premia huku Newcastle ikiongoza mbio za kumnasa Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 20. (Gazetta dello Sport – In Itali)

Manchester United inaweza kuwauza kiungo wa kati wa Uingereza Jadon Sancho, 23, na kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, kwa Juventus kwa £26m pekee. (The Sun)

Sir Jim Ratcliffe, ambaye bado hajakamilisha mpango wa kuchukua shughuli za soka katika Manchester United, tayari yuko kwenye majadiliano kuhusu mustakabali wa mshambuliaji Mwingereza anayecheza kwa mkopo Mason Greenwood, 22. (Caught Offside)

Beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 23, "amesalia kuwa mgombea" kwa uhamisho wa majira ya baridi kutoka Nice kwenda Manchester United. (Sky Sports Germany)

Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo anasema fowadi wa Ureno Joao Felix, 24, atarejea katika klabu hiyo ikiwa Barcelona wataamua kutofanya uhamisho wake wa mkopo Nou Camp kuwa wa kudumu. (Goal)

Kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 18 ataongeza mshahara wake maradufu - kutoka £10,000 hadi £20,000 - ikiwa atakuwa mchezaji wa kawaida kwenye kikosi cha kwanza. (Star)

Baadhi ya wachezaji wa Everton wanaweza kuomba fidia kutoka kwa klabu hiyo kwa kupoteza mapato yao iwapo watashuka daraja, kufuatia adhabu ya pointi 10 ya Toffees kwa ukiukaji wa kanuni za fedha. (The sun)

Nottingham Forest inaweza kukabiliwa na vikwazo vya uhamisho wa Januari juu ya malipo ya ada ya kuchelewa inayodaiwa na mawakala. (The Sun)

West Ham wanatazamiwa kutuma maombi ya kuongeza uwezo wa Uwanja wa London hadi kubeba watu 68,000 siku za mechi, jambo ambalo litaufanya kuwa uwanja wa pili kwa ukubwa katika Premier League nyuma ya Old Trafford. (The Mail)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
16m ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
38m ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
1h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
2h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
2h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
5h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
7h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
8h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
8h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
10h ago
READ MORE β†’