Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Disemba 07 2023

Joel JJ By Joel JJ
7 Dec 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Disemba 07 2023

Real Madrid wako tayari kumpa mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe kandarasi mwezi Januari kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa msimu ujao, lakini wababe hao wa Uhispania watampa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hadi Januari 15 kukubali au kukataa. (AS - In Spanish)

Mshambulizi wa Brazil Richarlison analengwa na klabu za Saudi Pro League lakini Tottenham hawana uwezo wa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 isipokuwa wanaweza kurejesha angalau pauni milioni 60 walizolipa kumsajili kutoka Everton. (90 min)

Tottenham wanafikiria kumsajili beki wa Everton na England Ben Godfrey, 25, mwezi Januari. (Sports) Manchester City na Manchester United zote zinamtaka mlinzi wa Lille mwenye umri wa miaka 18 Mfaransa Leny Yoro, ambaye mkataba wake katika klabu hiyo ya Ligue 1 utaendelea hadi Juni 2025. (Le10 Sport - in French)

Juventus wako tayari kujiondoa katika mpango wa kumsajili fowadi wa Manchester United na Uingereza Jadon Sancho, 23. (Tuttosport - in Italian)

Mshambulizi wa Chelsea na Uingereza Noni Madueke, 21, ana nia ya kuondoka katika klabu hiyo ya London kwa vile hajafurahishwa na hatua ya kutochezeshwa katika klabu hiyo (TeamTalk)

Kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard na meneja wa zamani wa Aston Villa Dean Smith wanashindana kuchukua mikoba ya Charlotte FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka. (Subscription Required)

Beki wa Newcastle United Tino Livramento, 21, anafuzu kuchezea Scotland na Ureno lakini anataka kuthibitisha kuwa anatosha kuichezea Uingereza. (Telegraph – Subscription Requiired)

Liverpool wamemsaka fowadi wa Benfica na Uholanzi Kyanno Lorenzo Silva, 18. (Football Insider)

Iwapo West Ham wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan na Uturuki Hakan Calhanoglu, 29, watalazimika kulipa zaidi ya £40m. (Calciomercato – In Italy)

Meneja wa Nottingham Forest Steve Cooper, 43, amewaambia marafiki zake kwamba amesikia mapendekezo ya kufutwa kazi na klabu hiyo. (Football Insider)

AC Milan wako tayari kuongeza hamu ya kumnunua mlinzi wa Arsenal Jakub Kiwior na wako tayari kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 23 kwa mkopo ikiwa na lengo la kumnunua. (90 min) Arsenal wanamfuatilia kiungo wa kati wa Marekani na Hajduk Split Rokas Pukstas, 19. (Sun)

Kipa wa Ufaransa Mike Maignan, 28, huenda asitie saini mkataba mpya na AC Milan huku Manchester United, miongoni mwa klabu nyingine za Ulaya, wakionyesha nia. (Corriere della Sera – In Italy)

BBC

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
54m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
57m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →