Mkufunzi wa Simba Abdelhak Benchikha ameingia tatu bora katika kinyan'ganyiro cha kuwania tuzo ya Kocha bora wa mwaka wa CAF
Benchikha anawania tuzo hiyo itakayotolewa Disemba 11 nchini Morocco baada mafanikio aliyoipa USM Alger
Msimu uliopita Benchikha aliiongoza USM Alger kutwaa kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) kisha kuiongoza timu hiyo kushinda Super Cup kwa ushindi dhidi ya Al Ahly
Anachuana na Walid Regragui wa timu ya Taifa ya Morocco na Aliou Cisse wa timu ya Taifa ya Senegal