Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ili wawe nafasi ya kutinga raobo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Medeama Fc
Kesho Ijumaa Yanga itashuka uwanja wa Baba Yara kumenyana na Medeama katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku kwa saa za Tanzania (saa 10 jioni Ghana)
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi alisema wanafahamu mchezo huo utakuwa mgumu lakini njia pekee wao kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali ni lazima washinde
"Ni lazima tushinde mechi yetu ya kesho mbele ya Medeama ili tufuzu hatua inayofuata. Najua sio rahisi ila tutaweza kesho kupata alama"
"Tumepata alama moja kwenye kundi ila timu yetu imefanya vizuri kwenye michezo iliyopita"
"Leo ndio nitajua kwenye maandalizi yetu ya mwisho nini nitaenda kufanya ila alama tatu za kesho ni lazima kwa sababu ni muhimu kwetu," alisema Gamondi



