Yanga - Local

Yanga ugenini dhidi ya Medeama leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Dec 2023
Yanga ugenini dhidi ya Medeama leo

Jioni ya leo Yanga itakuwa uwanja wa Baba Yara katika Mji wa Kumasi kuikabili Medeama Fc katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya tatu kundi D

Hii ni mechi muhimu sana kwa Yanga kuzisaka alama zote tatu huko ugenini katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jana, Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi aliweka wazi kuwa kikosi chake leo kitashuka dimbani wakiwa na dhamira moja, kusaka ushindi

Yanga imedhamiria kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, ili kufanikisha hilo Wananchi wanahitaji kukusanya angalau alama 9 kutoka mechi nne zilizosalia

Kama Yanga itashinda leo, itafikisha alama nne huku ikiwa na mechi mbili nyumbani ambazo kama itashinda itafikia malengo ya alama 10

Hautakuwa mchezo rahisi kwa kuwa hata Medeama Fc wana hesabu zao za kushinda mechi zote nyumbani

Walishinda mchezo uliopita dhidi ya CR Belouizdad na leo watashuka tena uwanjani kusaka ushindi wa pili

Kwa hakika zitakuwa dakika 90 za kutoka jasho jingi kwa wachezaji wa Yanga ili kuhakikisha ushindi unapatikana na kama sio ushindi basi hata sare lakini sio kupoteza mchezo huo kwani wakipoteza watafifisha matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’