Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Disemba 10 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Dec 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Disemba 10 2023

Kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips, 28, yuko kileleni mwa orodha ya wanunuzi wa Manchester United msimu ujao wa joto. (Sun)

Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa RB Leipzig na Ubelgiji Lois Openda, 23, wakati wakitafuta kuchukua nafasi ya winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, na mhambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 28, msimu ujao. (Mirror)

Rais wa Barcelona Joan Laporta anapanga kufanya mazungumzo kuhusu mustakabali wa wachezaji wawili wa Ureno Joao Felix, 24, kwa mkopo kutoka Atletico Madrid, na Joao Cancelo, 29, kwa mkopo kutoka Manchester City. (Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa Reading mwenye umri wa miaka 18, Caylan Vickers yuko tayari kuhamia kwa miamba ya Uhispania Real Madrid. (Sun)

Everton wamekataa ofa kutoka Tottenham ili kubadilisha masharti ya mkataba wa pauni milioni 10 uliokubaliwa kama sehemu ya uhamisho wa kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Dele Alli, 27, kwenda Goodison Park Januari 2022. (Times)

Bayern Munich wamemfanya mchezaji wa Barcelona Ronald Araujo, 24, kuwa mlengwa wao mkuu wa uhamisho na wanaweza kulipa ada "kubwa" kwa mlinzi huyo wa Uruguay. (Sky Sports Ujerumani)

&Mshambuliaji wa zamani wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, ambaye alistaafu mwishoni mwa msimu uliopita, anasema "anazungumza" na AC Milan kuhusu kurejea katika klabu hiyo katika baadhi ya nafasi. (Sky Sports Italia)

Juventus wanafuatilia hali ya kiungo mshambuliaji wa Brazil Felipe Anderson, 30, ambaye kandarasi yake huko Lazio inakamilika msimu wa joto. (Calciomercato)

Manchester United wainaongoza Tottenham katika kinyang'anyiro cha kumsajili mlinzi wa Nice wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 23. (Football Insider)

Newcastle wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Crystal Palace wa Uingereza Sam Johnstone, 30. (Star)

Manchester City wanavutiwa na mlinzi wa Club Brugge Tajon Buchanan mwezi Januari na watalazimika kulipa takribani pauni milioni 50 kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada mwenye umri wa miaka 24. (Star)

Newcastle United wanapanga kufanya usajili wa mkopo kutoka Saudi Pro League mwezi Januari. (Football Insider)

Wolves wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 7 mwezi Januari kwa kiungo wa kati wa Burnley Muingereza Josh Brownhill, 27. (Mirror)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’