Mshambuliaji Victor Osimhen wa Nigeria ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2023 katika hafla ya utoaji wa tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) iliyofanyika jana mjini Marrakesh
Mchezaji huyo wa Napoli aliwashinda Mohamed Salah na Achraf Hakimi wa Morocco. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mnigeria kutwaa taji hilo tangu Nwankwo Kanu mwaka 1999
Ulikuwa usiku wa furaha kwa Nigeria kwani Asisat Oshoala alishinda tuzo kama hiyo upande wa wanawake ikiwa ni mara ya sita kwa nyota huyo wa Barcelona kushinda tuzo hiyo

Washindi hupigiwa kura na jopo linalojumuisha kamati ya ufundi ya Caf pamoja na wanahabari wa Afrika, makocha wakuu na manahodha
Vilabu vinavyoshiriki katika hatua ya makundi ya mashindano ya bara Afrika pia vina usemi kuhusu mshindi wa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wachezaji wanaocheza soka barani Afrika, Percy Tau wa Afrika Kusini alishinda tuzo hiyo ambayo mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Mayele alikuwa akishindania pia