Simba - Local - Transfer

Matola apewa kazi maalum Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Dec 2023
Matola apewa kazi maalum Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha, raia wa Algeria ambaye alitua na msaidizi wake Farid Zemiti na kocha wa viungo Kamal Boudjenane amempa mzawa, Seleman Matola jukumu la kupendekeza na kusajili wachezaji wazawa kwenye dirisha hili la Januari.

Matola ambaye ana mkataba wa kuifundisha timu ya vijana ya Simba, alirudishwa timu kubwa baada ya kuondolewa kwa kocha Robertinho Oliveira hivyo uongozi wa Simba ulimpa nafasi hiyo Matola na Daniel Cadena kukaimu hadi walipompata kocha mpya.

Habari za ndani katika uongozi wa Simba ni kuwa Benchikha ameridhia kumpa jukumu hilo Matola ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, kwani anawajua vizuri wachezaji wa ndani zaidi yake na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba pia imebariki suala hilo.

Matola atashirikiana na Cadena kuandaa ripoti nzima ya kikosi na kutoa mapendekezo ya nani abaki na nani waachane nao katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo unaofunguliwa rasmi Desemba 16, mwaka huu

Benchikha anaendelea kukifanyia tathmini kikosi chake lakini ni wazi katika dirisha dogo la usajili kuna nyota wapya wachache wataongezwa lakini usajili mkubwa zaidi utafanyika katika dirisha kubwa litakalofunguliwa Juni/Julai 2024

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
29m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’