Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Disemba 14 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Dec 2023
Tetesi za soka Ulaya, Disemba 14 2023

Manchester United wako hatarini kumpoteza Mfaransa Raphael Varane, 30, kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao huku kandarasi yake ikitarajiwa kumalizika mwaka mmoja mapema kuliko ilivyotangazwa hapo awali. (Athletic- Usajili unahitajika)

Barcelona na vilabu vingine vikubwa vya Ulaya vinamfuatilia mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Mason Greenwood, 22, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo wa msimu mmoja huko Getafe. (Talksport)

Napoli wamefanya mazungumzo na klabu ya mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen kuhusu kuongeza mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hadi 2026, ikiwa ni pamoja na kipengele cha kumuachilia cha takriban £115m. (Sky Sports Italia)

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag hayuko hatarini kutimuliwa kwani klabu hiyo haitaki kufanya maamuzi yoyote makubwa hadi mauzo yanayotarajiwa ya 25% ya klabu kwa shirika la Ineos la Sir Jim Ratcliffe kutatuliwa. (Independent)

Hata hivyo, mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Ten Hag katika klabu ya Manchester United. (Sun)

Kocha wa zamani wa Wolves Julen Lopetegui pia yuko katika nafasi nzuri ya kurithi mikoba ya Ten Hag ikiwa klabu hiyo ya Old Trafford itaamua kuachana na Mholanzi huyo. (Relevo - kwa Kihispania)

AC Milan wapo kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu mkataba wa mkopo kwa beki wa Poland Jakub Kiwior, 23. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Beki wa Borussia Monchengladbach na Uswizi Nico Elvedi, 27, ameonekana kulengwa na Chelsea Januari kufuatia jeraha lingine kwa beki wa pembeni wa Uingereza Reece James, 24. (Teamtalk)

Kushindwa kwa Manchester United kufuzu kwa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa kumeacha pengo la £28m katika bajeti yao ya uhamisho na huenda ikamaanisha kuwa wako tayari kupokea maombi ya kuwamuuza kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 31, mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 28, na Varane. (Mail)

Chelsea wako tayari kumuuza beki wa Uholanzi Ian Maatsen, 21, wakati wa uhamisho wa mwezi ujao. (Mirror)

Aston Villa huenda wakamsajili kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg na Israel Oscar Gloukh mwenye umri wa miaka 19 mwezi Januari kwa hadi £50m. (Football Insider)

Wolves wamekubali mkataba mpya kwa mshambuliaji wa Korea Kusini Hwang Hee-chan, 27, hadi Juni 2028 kukiwa na chaguo la msimu zaidi. (Fabrizio Romano)

Everton, Burnley na Leeds United ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia beki Mwingereza Archie Brown, 21, anayechezea Gent. (Mail)

BBC

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’