Hersi apata uteuzi mwingine AFCON

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th December 2023


Hersi apata uteuzi mwingine AFCON

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limemteua Mwenyekiti wa Shirikisho cha Klabu Afrika (ACA) na Rais wa Yanga, Hersi Saidi kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi za Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani (Chan)

Hilo limesemwa leo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia katika mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaoendelea mjini Iringa

Karia amesema kuwa Hersi ameteuliwa kuingia katika kamati hiyo kwa vile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF nafasi aliyoipata baada ya kuukwaa uongozi wa ACA

"Kwa nafasi ya kuwa Rais wa klabu Afrika, Hersi Said ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na hivyo ameingia kwenye Kamati ya Maandalizi ya Chan na Afcon," alisema Karia

Ilikuwa ni suala la muda kwa Hersi kuanza kuonekana katika majukumu makubwa ya uongozi wa soka Afrika baada ya kazi nzuri aliyofanya tangu akabidhiwe mikoba ya kuiongoza klabu ya Yanga


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.