Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Disemba 16 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th December 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Disemba 16 2023

Chelsea inaweza kusaini mkataba na mlinda lango wa Arsenal na Uingereza Aaron Ramsdale, 25, baada ya kuthibitishwa kuwa mlinda mlango wa Blues Robert Sanchez atakuwa nje ya uwanja kutokana na jeraha la goti. (Talksport)

Barcelona inaweza kumuuza mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 35, msimu huu ili kusaidia kufadhili uhamisho wa kiungo wa kati wa Newcastle kutoka Brazil Bruno Guimaraes mwenye umri wa miaka 26. (Football Transfers)

Real Madrid wanamfuatilia kaka mdogo wa Jude Bellingham Jobe baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 kuonyesha kuwa na mwanzo mzuri wa soka wa miaka 18 huko Sunderland (90Min)

West Ham wanatarajia kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Pablo Fornals, 27, ili kusaidia matumizi yao ya Januari, huku The Hammers wakitamani kuwasajili mabeki wawili na mshambuliaji. (90Min)

Tottenham wanapanga kumsaka mlinzi wa Benfica Mbrazil Morato, 22, baada ya kuwavutia mawakala waliomtazama katika mechi dhidi ya RB Salzburg katika Ligi ya Mabingwa katikati mwa juma. (Sun)

Chelsea wanajiandaa kwa pambano la pauni milioni 34 na wababe wa Italia Juventus, kupata saini ya Torino na mlinzi wa Italia Alessandro Buongiorno, 24 kutoka (Sun)

Kiungo wa kati wa Marekani Brenden Aaronson, 23, anaweza kukatisha mkata wake wa mkopo katika Union Berlin na kurejea katika klabu yake mama Leeds mnamo Januari kwa sababu ya kukosekana kwa soka la kawaida la kikosi cha kwanza. (Teamtalk)

Liverpool wanakabiliwa na ushindani kutoka Newcastle, na AC Milan wa Roma kwa ajili ya kumnunua mlinzi wa Equador na Bayer Leverkusen Piero Hincapie mweney thamani ya £60m (Bild - in German, subscription required)

Manchester United haitafanya uamuzi kuhusu mustakabali wa Erik ten Hag kama meneja hadi mkataba wa uwekezaji wa Sir Jim Ratcliffe ukamilike, hata kama wamepata kushindwa vibaya na Liverpool siku ya Jumapili. (Football Insider)

Luka Modric anatarajiwa kuondoka Real Madrid mwisho wa msimu huu kwani klabu hiyo haitarajiwi kutoa ofay a mkataba mpya kwa kiungo huyo wa zamani wa Croatia mwenye umri wa miaka 38. (Sport - in Spanish)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.