Yanga imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji Shekhan Ibrahim Khamis aliyesajiliwa kutoka klabu ya JKU
Kwa takribani siku nne usajili wa Shekhan ulitawala mitandao ya kijamii kutokana na vile usajili huo ulivyokamilishwa na Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji
Shekhan ametua Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu na anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili
Nyota huyo anatarajiwa kutambulishwa kwa mashabiki wa Yanga kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ambao Yanga watacheza na Mtibwa Sugar baadae leo katika uwanja wa Azam Complex



