TFF - Local

Nyamlani aongezwa miaka miwili TFF

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Dec 2023
Nyamlani aongezwa miaka miwili TFF

Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika jana mkoani Iringa, umeridhia makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho hilo, Athuman Nyamlani kuendelea na wadhifa huo

Kwa mujibu wa katiba ya TFF, muda wa mjumbe wa kuteuliwa wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo ni miaka miwili hivyo Nyamlani kwa vile alishika wadhifa huo baada ya kuteuliwa na Rais wake Wallace Karia amemaliza muda wake mwaka huu

Kikatiba, ilipaswa Karia atangaze kumteua kwa mara ya pili, Nyamlani na kisha wajumbe wa mkutano mkuu kupitisha, jambo ambalo lilifanyika na hivyo ataendelea kuhudumu katika nafasi hiyo ambayo pia inamfanya awe mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango ya TFF

"Na kwa vile alikuwa naye ni miongoni mwa wajumbe niliowateua, nilikuwa nawaomba wajumbe mridhie Athuman Nyamlani aendelee kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa TFF," alisema Karia

Baada ya Karia kutangaza hivyo, wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF walipitisha uteuzi huo na hivyo Nyamlani ataendelea kuhudumu kwa miaka miwili ijayo. Mbali na Nyamlani, wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF, wamepitisha uteuzi wa Ahmed Mgoyi, Said Soud na Hawa Mniga kuwa wajumbe wa kuteuliwa wa kamati ya utendaji ya TFF.

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’