Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanatambua kazi iliyo mbele yao katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama Fc ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi alisema wanahitaji kuwek hai matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata ya michuano hii hivyo wanahitaji ushindi
"Tumejiandaa vizuri kwa ajili huu mchezo muhimu sana kwetu, tunahitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata katika michuano hii"
"Tumekuwa na muda mzuri wa kufanya mazoezi, nawaamini wachezaji wangu, kesho tutakuwa na mchezo mzuri dhidi ya Medeama hapo kesho,"alisema Gamondi
Gamondi amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao katika mchezo ambao wamedhamiria kushinda
"Mashabiki wa Yanga wamekuwa nasi kila htua tangu mwanzoni mwa msimu, kesho ni mchezo muhimu tunawaomba waje kwa wingi, wachezaji wameahidi watafurahi baada ya dakika 90," aliongeza Gamondi
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage amesema wachezaji wote wako tayari na kila mmoja anafahamu alama tatu pekee zitawaweka katika nafasi nzuri katika kundi
"Sisi wachezaji tuko tayari, tunafahamu umuhimu wa mchezo huu, tunahitaji ushindi ili kuwa na matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata"
"Makocha wamefanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita hivyo tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Medeama hapo kesho," alisema



