Real Madrid huenda wakataka kumsajili tena beki wa Manchester United Raphael Varane, 30, baada ya beki wa Austria David Alaba, 31, kupata jeraha baya. (Cadena Cope - kwa Kihispania)
Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anataka kusalia na Varane, ambaye alijiunga na Red Devils kutoka Real mwaka 2021, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 31, katika dirisha la uhamisho la Januari. (ESPN)
Arsenal wameipiku Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney mwenye umri wa miaka 27 kutoka Brentford. (Independent)
Manchester United wanavutiwa na winga wa Real Sociedad wa Japan Takefusa Kubo, 22, kama mbadala wa winga wa Brazil Antony, 23. Kubo amefunga mabao sita na kusaidia kufunga mara tatu katika La Liga msimu huu. (Sun)
Vilabu vya ligi kuu ya Ujerumani Bayer Leverkusen, RB Leipzig na Stuttgart vinatafuta dili la kumsajili winga wa Manchester United na England Jadon Sancho, 23. (90 Min)
Juventus wanaweza kuwa na faida kidogo dhidi ya Newcastle United katika juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City Kalvin Phillips kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anataka kujua kuhusu muda wa kucheza atakaopata kabla ya kuamua ni klabu gani ya kujiunga nayo, huku kukiwa na uwezekano wa kupata nafasi zaidi nchini Italia. (Telegraph - usajili unahitajika)
Brentford, Brighton na Nottingham Forest wanavutiwa na mshambuliaji wa Hoffenheim mwenye umri wa chini ya miaka 21 wa Hoffenheim Maximilian Beier. Liverpool na Bayer Leverkusen pia wanamfuatilia mchezaji huyo. (Christian Falk kwenye X)
Chelsea hawana nia ya kumsajili kipa wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale, 25, mwezi Januari. Ramsdale amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kuondoka baada ya kuanza mechi mara tano pekee za Ligi Kuu msimu huu. (Fabrizio Romano kwenye X)
Ramsdale hata hivyo hataruhusiwa kuondoka Arsenal Januari, licha ya kukosa muda wa kucheza. (Football Insider)
Everton wameweka bei ya pauni milioni 100 -kiasi kinachovunja rekodi kumnunua mlinzi wa England aliye chini ya umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite, 21, huku Manchester United na Tottenham zikimtaka. (i newspaper)
Kiungo wa kati wa Fluminense wa Brazil Andre, 22, amesisitiza nia yake ya kutaka kucheza katika Ligi ya Premia huku Fulham ikitaka kumsajili. (Standard)
Tottenham wana nia ya kumnunua beki wa Uingereza Tosin Adarabioyo na wanaweza kumnunua mwezi Januari, lakini Fulham wanatumai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ataongeza mkataba wake nao hadi msimu ujao wa joto. (Standard)
Tottenham wameanza mazungumzo ya kumsajili beki wa Nice Jean-Clair Todibo mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari, huku Manchester United pia wakihusishwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (Talksport)
Steve Cooper, ambaye alifutwa kazi na Nottingham Forest siku ya Jumanne, anagombea nafasi ya Roy Hodgson wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 76 atakapoondoka Crystal Palace. (Standard)
BBC