Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Disemba 24 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Dec 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Disemba 24 2023

Fulham itadai ada ya hadi £60m mwezi Januari kwa ajli ya kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, ambaye amekuwa akihusishwa na Bayern Munich, Liverpool na Arsenal. (Football Insider)

Arsenal wamewasiliana na wawakilishi wa Ivan Toney wanapofikiria kutoa ofa thabiti kwa Brentford kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 27. (Rudy Galetti)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe hataki kuondoka Paris St-Germain mwezi Januari licha ya kwamba kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 itakamilika mwishoni mwa msimu. (L'Equipe)

PSG wana makubaliano ya mdomo kumsajili Lucas Beraldo anayelengwa na Liverpool, huku mlinzi huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 20 akitarajiwa kuondoka Sao Paulo kwa pauni milioni 17 mwezi Januari. (Fabrizio Romano via Goal)

Inter Milan wana matumaini ya kuipiku Manchester City katika kuinasa saini ya mshambuliaji wa Canada Tajon Buchanan wa Club Bruges, 24. (Gazzetta dello Sport)

Strasbourg wanafikiria kumnunua mlinzi wa kushoto wa Boca Juniors wa Argentina, 19, Valentin Barco, ambaye pia analengwa na Chelsea Januari. (Evening Standard) Brighton pia wameonyesha nia na Barco na wamekutana na wawakilishi wake. (TYC Sports )

Arsenal wamemuongeza kiungo wa kati wa Sao Paulo Mbrazil Pablo Maia, 21, kwenye orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuwindwa Januari. (Football transfers)

Tottenham wanamfuatilia Radu Dragusin baada ya kutuma maskauti kumtazama mlinzi huyo wa Romania, 21, akiichezea Genoa dhidi ya Juventus wiki iliyopita. (Fabrizio Romano)

Lyon inamlenga mlinzi wa West Ham na Algeria, Said Benrahma, 28, mwezi Januari. (Sport)

Aston Villa wameungana na Tottenham katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Juventus Samuel Iling-Junior, 20, kwa dau la takribani pauni milioni 17 huenda likatosha kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 21. (Football Insider)

Barcelona wana nia ya kumbakisha mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 24, hadi msimu huu lakini watafuatilia mkataba mwingine wa mkopo kwa vile hawawezi kumudu uhamisho wa kudumu. (Goal)

West Ham wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa Bayer Leverkusen wa Ujerumani Jonathan Tah, 27, ambaye anapendelea kuhamia Ligi ya Premia kuliko Bayern Munich. (Bild)

Lille wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Southampton mwenye umri wa miaka 21 wa Ufaransa Sekou Mara mwezi Januari. (L'Equipe )

Beki wa Barcelona na Uruguay Ronald Araujo, 24, anataka kusalia na mabingwa hao wa La Liga huku Bayern Munich wakimtaka. (Sky Sports Germany)

Tottenham na Monaco wanataka kumsajili mlinzi Muingereza Tosin Adarabioyo, 26, kwa uhamisho wa bure mkataba wake wa Fulham utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (90 min)

Newcastle wanamaliza mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Uingereza Joe White na Crewe ili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ajiunge na Stockport County kwa msimu uliosalia kwa mkopo. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’