Baada ya kurejea jijini Dar es salaam wakitokea Dodoma, wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya siku chache
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema wachezaji ambao hawatakuwa na majukumu ya timu za Taifa watarejea kambini Disemba 30 tayari kwa safari ya Zanzibar kushiriki kombe la Mapinduzi
Harrison amedokeza kuwa kikosi cha Yanga kitakachoelekea visiwani Zanzibar huenda kikajumuisha baadhi ya wachezaji wapya
"Baada ya kurejea jijini Dar es salaam wachezaji wamepewa mapumziko ya siku chache. Tunatarajia kuondoka Dar Disemba 30 kwenda Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi"
"Msafara wetu utajumuisha wachezaji ambao hawatakuwa na majukumu ya timu za Taifa. Tunakwenda Zanzibar tukiwa na dhamira moja, kwenda kuwapa furaha mashabiki wetu tukiwa na malengo ya kuwa mabingwa"
"Huenda tukawa na surprise ya wachezaji wapya huko Zanzibar," alisema Walter
Mchezo wa kwanza ni dhidi ya Bandari Fc ukitarajiwa kupigwa Disemba 31



