Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Disemba 29 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Dec 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Disemba 29 2023

Arsenal wanavutiwa na mlinzi wa Bayern Munich Mholanzi Matthijs de Ligt, 24, ingawa kuna uwezekano wa makubaliano yoyote kufanyika msimu huu wa joto. (Athletic)

Arsenal lazima iwashushe wachezaji kabla ya kusajili Januari na kocha Mikel Arteta huenda akatanguliza mikataba ya mkopo. (Mirror)

Mustakabali wa Roy Hodgson kama kocha wa Crystal Palace hauna uhakika kwani wanafikiria kumnunua Steve Cooper, ambaye alitimuliwa na Nottingham Forest mwezi huu. (Telegraph)

Mkataba wa kubadilishana unaohusisha mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 23, na mshambuliaji wa Chelsea wa Ubelgiji Romelu Lukaku, ambaye yuko kwa mkopo Roma, unaweza kufanyika mwaka ujao. (Tuttosport)

Nottingham Forest wapo kwenye mazungumzo ya juu na Monaco kuhusu kumnunua winga wa Ureno, Gelson Martins, 28. (L'Equipe)

Juventus itaweka kipaumbele usajili wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg mwenye umri wa miaka 28 mwezi Januari. (Calciomercato)

Manchester City itamruhusu kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, kujiunga na Newcastle kwa mkopo. Anatazamiwa kukataa kuhamia Juventus. (Sport)

Chelsea wamekubali dili la kumnunua kiungo wa kati wa Senegal chini ya umri wa miaka 17 Pape Daouda Diong kutoka klabu ya Senegal ya AF Darou Salam atakapofikisha umri wa miaka 18 mwezi Juni. (Fabrizio Romano)

Tottenham wanataka kusajili mlinzi wa kati ifikapo katikati ya Januari, huku mlinzi wa Nice ya Ufaransa Jean-Clair Todibo, 23, akiongoza orodha yao ya walioteuliwa. (Teamtalk)

West Ham wako tayari kumuuza mlinzi wa Morocco Nayef Aguerd mwenye umri wa miaka 27 mwezi Januari, huku klabu kadhaa za Saudi Arabia zikiwa na nia ya kumnunua. (Football Insider)

Eintracht Frankfurt wanataka kumsajili mshambuliaji wa Wolves wa Austria Sasa Kalajdzic, 26, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Bild)

Kiungo wa zamani wa Ufaransa Yann M'Vila yuko tayari kurejea Sunderland. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ni mchezaji huru baada ya kuondoka Olympiakos mwishoni mwa msimu uliopita. (Sunderland Echo)

Sevilla, Lyon na Freiburg wana nia ya kumsajili Hannibal Mejbri wa Manchester United mwenye umri wa miaka 20 kwa mkopo mwezi Januari. (Fabrizio Romano)

Mlinzi wa West Ham Thilo Kehre, 27, analengwa na Roma, ambao wanataka kumsajili beki wa kati mwezi Januari. (Corriere dello Sport) Manchester City wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumnasa kiungo wa kati wa River Plate Muargentina Claudio Echeverri, 17. (Sky Sports)

Echeverri anatazamiwa kukaa kwa muda katika klabu dada ya Manchester City ya Girona kabla ya kujumuishwa kwenye kikosi cha Pep Guardiola. (Mundo Deportivo)

Crystal Palace wanamtaka kiungo wa kati wa Sunderland mwenye umri wa miaka 21 Pierre Ekwah na mshambuliaji wa Ufaransa wa Paris St-Germain, Hugo Ekitike, 21. (Standard)

Liverpool wako tayari kumpeleka mlinzi Nat Phillips, 26, kwa mkopo tena mwezi Januari baada ya muda wake wa kuitumikia Celtic kuisha. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino, 32, anaweza kuondoka Al-Ahli baada ya miezi sita pekee, huku timu nyingine za Saudi Pro League Al-Shabab, Al-Ettifaq na Al-Fateh, Sheffield United na timu kutoka Uturuki zikimtaka. (Sport)

BBC

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’