Taarifa kutoka nchini Ghana zimebainisha kuwa winga wa Bechem United Augustine Okrah tayari amemalizana na Yanga
Wakati Wananchi wakisubiri utambulisho wa mchezaji mpya visiwani Zanzibar, imeelezwa kuwa Okrah tayari yuko Zanzibar
Okrah ndiye kinara wa mabao Ligi kuu ya Ghana akipachika mabao tisa kwenye mechi 16 alizocheza msimu huu
Okrah amewahi kuitumikia Simba msimu uliopita akifunga mabao manner katika ligi kuu ya NBC
Anaweza kutumika katika michuano ya ligi ya mabingwa hivyo kama atasajiliwa na Yanga anaweza kuongezwa iwapo Wananchi watatinga robo fainali



