Baada ya utambulisho wake hapo jana, kiungo mshambuliaji Augustine Okrah amejiunga katika kikosi cha Kocha Miguel Gamondi kinachojiandaa na mchezo wa pili unaofuata kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi
Kesho Jumanne, Yanga itashuka tena uwanja wa New Amaan Complex kuikabili Jamus ya Sudan Kusini ukiwa ni mchezo wa pili kwa Yanga kundi C
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, kocha msaidizi wa Yanga, Mussa Ndaw alithibitisha kuwa Okrah yuko fit na anaweza kutumika hapo kesho
"Okrah yuko fiti na tuna mpango wa kumtumia kwenye mechi zijazo za michuano hii," alisema
Yanga ilimtambulisha kuwa mchezaji wao jana baada ya kukamilisha usajili wake kutoka klabu ya Bechem United ya Ghana
Okrah amewahi kuitumikia Simba kwa msimu mmoja na baadae mchezaji huyo kurejea Ghana





