Simba - Local

Benchikha ataka mshambuliaji Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Jan 2024
Benchikha ataka mshambuliaji Simba

Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amewataka viongozi wa Simba kuhakikisha wanakamilisha usajili wa mshambuliaji mpya kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 15

Baada ya kuiongoza Simba kutinga fainali ya kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Singida FG baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1, Benchikha amesisitiza kuwa bado Simba inahitaji mshambuliaji bora zaidi ya alionao

Mmoja wa viongozi wa Simba aliyeko kwenye jopo la usajili amefichua kuwa Benchikha amekuwa mkali kupita wakati mwingine wowote

Ametaka kujua mchakato wa usajili wa mastaa wawili anaowataka haswa pale kwenye safu ya mbele umefikia wapi huku akisisitiza mshambuliaji wa kati anatakiwa kutangulia fasta kwani waendako ni kugumu na hawawezi kutoboa kwa picha aliyoiona mpaka sasa kwenye Kombe la Mapinduzi.

Benchikha amewaambia haridhishwi na viwango vya washambuliaji wake wakiongoizwa na Jean Baleke na Mosses Phiri

Baleke amefunga mabao mawili ndani ya mechi tano alizocheza kwenye mashindano hayo huku Phiri akifunga bao moja.

"Kocha anataka matokeo mazuri zaidi anaona bado nguvu yetu kule mbele haimfurahishi tunapambana kutafuta mtu wa maana wa pale mbele ili hawa tulionao wawe watu wa kuja kuongeza kitu baadaye na sio kuwategemea kama chaguo la kwanza," alidokeza kiongozi huyo wa Simba

Benchikha akizungumzia mechi hiyo ya jana amesema kikosi chake kimecheza mechi moja ngumu ya ndani dhidi ya timu Bora ambayo imempa nafasi ya kujua maboresho zaidi ambapo Sasa anakwenda kutafanyia kazi.

"Hii ni mechi Moja ngumu dhidi ya timu Bora, ukipata kipimo cha namna hii kinakupa nafasi ya kujua kazi mnayofanya ina ubora wa namna gani au wapi mnatakiwa kuongeza kitu," amesema Benchikha

"Kuna maeneo tunahitaji kuongeza nguvu au Kuna wachezaji wanatakiwa kuongeza kasi ya kutupa ambacho timu inahitaji, changamoto yetu kubwa ipo hapa tutaendelea kufanya kazi ya kuboresha mambo ambayo tumeyabaini"

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’