Yanga - Simba - Azam - Singida - Local

Waamuzi watakiwa kuongeza umakini kombe la Mapinduz

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Jan 2024
Waamuzi watakiwa kuongeza umakini kombe la Mapinduz

Mjadala mkubwa ulioibuka katika mitandao ya kijamii ni matukio ya yaliyojiri kwenye kombe la Mapinduzi kwa waamuzi kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za soka na hivyo kuzinufaisha timu ambazo hazikustahili

Pengine katika michuano ya mwaka huu ndio imeshuhudia makosa mengi yakifanywa na waamuzi kuliko wakati mwingine wowote tangu michuano hiyo ilipoanzishwa

Jana Kamati ya waamuzi ya michuano hiyo ilitangaza kumfungia mwamuzi wa kwanza msaidizi Yusuf Shombe Issa kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria kwa kuruhusu bao la kwanza la Azam na baadaye Singida Fountain Gate ambayo hayakuwa halali katika mchezo wa robo fainali

Azam iliandika bao la kwanza kupitia kwa Alassane Diao kwa kichwa akionekana ameotea kabla ya Singida kupata bao la pili lililofungwa na Habib Kyombo akionekana pia ameotea na kufanya matokeo ya mwisho Singida kushinda 2-1 na kutinga nusu fainali

Mbali na Issa, pia Shekha alisema mwamuzi wa pili aliyefungiwa ni Mohamed Mwadini aliyekuwa mwamuzi wa kwanza msaidizi ambaye aliruhusu bao katika mchezo wa makundi kati ya JKU na APR akidai mpira ulivuka mstari wa goli wakati haikuwa hivyo

Mechi hiyo iliisha kwa APR kushinda mabao 3-1 na kwenda robo fainali ambako ilifanikiwa kuiondosha Yanga kabla ya kutolewa na Mlandege katika nusu fainali

Katika mchezo wa nusu fainali kati ya Singida FG dhidi ya Simba madudu mengine yakafanyika Singida FG wakipoteza mchezo huo kupitia mikwaju ya penati

Licha ya kuongezwa dakika 6 baada ya dakika 90 kumalizika, mchezo ulichezwa kwa takribani dakika 100 Simba ikisawazisha bao katika dakika ya 9 kati ya 10 zilizochezwa kupitia mpira wa kona ambao ulikuwa na utata

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Waziri Shekha amesema baada ya kikao kilichofanyika leo Januari 11, 2024 kupitia ufanisi uliofanywa mwamuzi Msomali na wasaidizi wake wamegundua kwamba mwamuzi huyo hakuwa sahihi kwenye uamuzi wake huo wa kuwapa kona Simba ambayo ilizaa bao la kusawazisha

Shekha amesema kosa hilo ni la kibinadamu kwani waamuzi nao hufanya makosa

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’