Michuano ya Afcon 2023 tayari imeanza Ivory Coast mpaka sasa baadhi ya mechi zikitoa matokeo yasiyotarajiwa na wengi
Katika mechi nne zilizochezwa mpaka sasa, mechi mbili zimetoa washindi huku mechi mbili zikimalizika kwa sare
Wenyeji Ivory Coast walianza vyema michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea Bissau
Mechi nyingine tatu zikapigwa jana, Guinea ya Ikweta ikapata sare ya bao 1-1 dhidi ya Nigeria katika mechi ambayo wengi waliamini Nigeria ingeshinda
Misri ikaponea chupuchupu mbele ya Msumbiji ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 huku Ghana wakiangukia pua mbele ya Cape Verde wakichapwa mabao 2-1
Leo mechi nyingine tatu zitapigwa ambapo Senegal watachuana na Gambia saa 11 jioni, Cameroon watachuana na Guinea saa 2 usiku na Algera wakichuana na Angola saa 5 usiku
Tanzania itatupa karata yake ya kwanza siku ya Jumatano kwa mchezo dhidi ya Morocco mchezo utakaopigwa saa 2 usiku
Kwa matokeo ya mechi hizi za mwanzo, unaweza kusema hakuna lisilowezekana, Tanzania nayo ina nafasi ya kupata matokeo dhidi ya Morocco
Kama wachezaji wa Stars watajitoa na kujituma kwa asilimia 100 kwa nini isiwezekane?