Uongozi wa klabu ya Simba umetimiza mapendekezo ya kocha Abdelhak Benchikha kwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji
Leo Simba imemtambulisha mshambuliaji Pa Omar Jobe raia wa Gambia
Jobe amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya FC Zhenis ya Kazakhstan
Ni usajili ambao ni 'surprise' kwani haukuwa tetesi nyingi, bila shaka kitengo cha scout cha Simba kimefanya kazi yake vyema kumnasa Mgambia huyu mwenye umri wa miaka 25